Posts

Showing posts from March, 2017

Watumishi wa umma nchini Tanzania wanaongoza kutokuwa na furaha!

Pigo jingine kwa walimu na watumishi wa umma kwa ujumla

Image
NA RUSTON MSANGI. Katika watumishi wa umma, ualimu ni kada pekee yenye watumishi wengi kuliko kada yoyote ile nchini. Ni kada mojawapo yenye changamoto nyingi pengine kuliko kada yoyote ile. Tangu utawala wa awamu ya 5 uingie madarakani chini ya Rais Magufuli, matatizo ya watumishi wa Umma hususani walimu yamekuwa maradufu ya mwanzo. Mtakumbuka kwamba tangu kuanza kwa zoezi la uhakiki usioisha, haki nyingi za walimu zimesimamishwa bila kufanyiwa kazi huku kukiwa na manyanyaso, ukandamizwaji na uonevu usio na mwisho kupitia kwa watendaji mbalimbali serikali kuu, halmshauri na baadhi ya maeneo kutoka kwa serikali za kata na vijiji. Madaraja ya mishahara yamesimama, uhamisho umesimama, ongezeko la mshahara (salary increment ) kwa mujibu wa mkataba wa kazi umesimama, madeni hayalipwi, makato yameongezeka maradufu. Mbali na yote hayo, walimu wameendelea kutimiza wajibu wao na hata kulaumiwa kwa matokeo mabovu ya shule za serikali. Kabla ya hata kupanda kwa  makato ya 15%

Walimu wa mwaka 1993 ni mfano wa kuigwa

NA RUSTON MSANGI. Katika historia ya harakati za walimu nchini, inaonesha kwamba mwaka 1993 kulitokea mgomo wa walimu. Kipindi hiki ulikuwa utawala wa awamu ya pili chini ya Rais Ally Hassan Mwinyi. Mgomo huu ulitokana na madai lukuki ya walimu dhidi ya Serikali, kama ilivyo sasa. Kinara wa mgomo huo alikuwa Mwalimu Peter Lebabu Mashanga, huyu alikuwa ni mwenyekiti wa OTTU (Organization of Tanzania Trade Unions) tawi la Azania sekondari. Mwalimu Peter Lebabu Mashanga akiungwa mkono na walimu wa Dar es Salaam mnamo October 1993, walimuandikia Rais Ally Hassan Mwinyi barua, wakieleza madai 14 ya walimu na kumpa muda maalum wa kutekeleza madai hayo. Vinginevyo wangegoma nchi nzima ikifika 1/11/1993 hadi madai yatakapotekelezwa. Madai haya ya walimu ya mwaka 1993 yalijulikana kama ''Pan African Tanzania Teachers Demands''. Na madai yenyewe baadhi ni kama ifuatavyo:- 1. Comprehensive medical care. 2. Emergency medical fund amounting to 60,000 p.m 3. Lunch