Posts

Showing posts from June, 2017

MEYA WA MANISPAA YA UBUNGO MH BONIFACE JACOB AZINDUA KITUO CHA KIPYA CHA KIELETRONIKI CHA KULIPA

Image
Mstahiki Meya Jacob Boniface akiwa katika uzinduzi Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ubungo, Boniface Jacob, leo Ijumaa 30 Julai 2017, amezindua kituo cha kisasa cha kukusanya kodi, ushuru na tozo mbalimbali katika eneo la Simu 2000. Hii itapunguza kero kwa  wananchi wanaoishi maeneo ya karibu na eneo la Simu 2000, kulipa kodi, ushuru na tozo mbalimbali ambapo awali walilazimika kwenda Kibamba zilizopo ofisi za Manispaa ya Halmashauri ya Ubungo. Kituo hiki kipya kinategemea kuwasaidia wakazi wa Sinza, Mabibo,  Makuburi, Ubungo na maeneo yote ya karibu.

BREAKING NEWS: MH EDWARD LOWASSA ATAKUWEPO MAKAO MAKUU YA JESHI LA POLISI LEO SAA SITA MCHANA

Image
Waziri Mkuu wa zamani Mh Edward Lowassa leo akuwepo Makao Makuu ya Jeshi la Polisi kujua hatma ya tuhuma zinazomkabili juu ya uchochezi .Mh Edward Lowassa anatarajia kufika makao makuu ya Jeshi la Polisi mnamo majira ya saa 6 mchana kama alivyoelekezwa na Jeshi hilo hilo la Polisi.,Inasemekana atasindikizwa na Polisi kutoka nyumbani kwake hadi makao makuy ya jeshi la polisi. Endelea kufuatilia kwa karb upate habari zaidi

SULEIMAN MATHEW ALIMAARUFU MESI NA MWENZAKE WAPETA KATIKA HUKUMU YA RUFAA

Image
Na Nkatunga Philibert Mahakama Kuu Kanda ya Mtwara imewaachia huru Suleiman Mathew (Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Lindi) na mwenzake Ismail Kupilila (Katibu wa CHADEMA Tawi la Nyangamara). Viongozi hawa walikuwa wamehukumiwa adhabu ya kifungo miezi nane jela bila faini na Mahakama ya Wilaya ya Lindi mnamo 18.01.2017. Baadae walikata rufaa Mahakama Kuu na kuomba dhamana kwa hati ya dharua ambayo walipewa tarehe 07.03.2017. Wakati anasoma hukumu hiyo Jaji Mlacha alisema kwamba kosa la kusanyiko lisilo halali linatakiwa kufanywa na watu watatu au zaidi sio wawili. Akasema pia kwamba vifungo vyao vimefutwa. Wako huru kwa sababu hawana hatia. Aliongeza kusema kwamba ameona mambo kadha katika kesi hii (Observations) 1. Kwa mujibu wa sheria Jeshi la Polisi halina mamlaka ya kutoa vibali kwa vyama vya siasa kuhusu mikutano au maandamano kama ambavyo aliyekuwa OCD Ngiichi alidai katika ushahidi wake. 2. Warufani wameelekezwa kutoa taarifa Polisi kama sheria inavyotaka na si kwa Mtendaji