Vyama vya wafanyakazi vijifunze kwa Kituo cha Sheria na Haki za binadamu LHRC!
NA RUSTON MSANGI. Ni jukumu la kila chama cha wafanyakazi nchini kusimamia, kulinda, kuboresha maslahi, na kuhakikisha haki za wanachama wake hazivunjwi, wala kukiukwa kwa namna yoyote ile. Majukumu hayo ya chama chochote cha wafanyakazi hayaepukiki kwa kuwa wanachama huwa na utaratibu maalumu wa kuchangia kwa njia ya ada, ili kufanikisha shughuli za chama husika. Mfano wa vyama vya wafanyakazi nchini ni kama Chama cha walimu Tanzania (CWT), Muungano wa wafanyakazi katika sekta ya viwanda na biashara (TUICO), Umoja wa wafanyakazi wa afya wa serikali (TUGHE), Muungano wa wafanyakazi wa Serikali za mitaa (TALGWU). Mwezi huu umekuwa ni pigo kwa wafanyakazi nchini, hasa wale walionufaika na mikopo ya elimu juu wakati wa masomo yao. Maumivu haya makubwa ni kuhusu mabadiliko ya sheria yaliyopelekea kuongezeka kwa makato ya marejesho ya mikopo, kutoka 8% ya awali hadi 15% iliyoanza kukatwa mwezi huu wa pili. Suala hili kiukweli limewaacha wafanyakazi wengi nchini na maumivu mak