Wakuu wa shule wapata nafasi ya kukomoa walimu.
NA RUSTON MSANGI. Ni wiki kadhaa sasa walimu wengi nchini wamekuwa katika msongo wa mawazo, hii ni kutokana na agizo la serikali linalotaka walimu wa sekondari wa stashahada na shahada wanaosemekana ni wa ziada kwa masomo ya sanaa wapelekwe shule za msingi. Mapema sana nilionesha kutokukubaliana na agizo hili kwa kuwa ni kimyume na mkataba, humuathiri mwalimu kisaikolojia, humshusha mwalimu cheo, hunyima wahusika ajira, nk. Katika utekelezaji wa agizo hili ambalo limepingwa na walimu wengi wenye akili, kumezuka matatizo makubwa zaidi. Baadhi ya wakuu wa shule za sekondari nchini wamepata nafasi ya kuonyesha chuki za wazi kabisa kwa walimu. Hii ni kutokana na ukweli kwamba kwa namna moja au nyingine wakuu wa shule wamehusika moja kwa moja katika zoezi la kuhamisha walimu kutoka sekondari kwenda shule za msingi. Na ushiriki wa wakuu wa shule haujawa wa heri wala haki, bali imekuwa ni nafasi kwao kuadhibu, kukomoa na kuondoa watu ambao wanahisi ni kero kwao. Nayasema hay