Posts

Showing posts from October, 2017

Uhakiki unatumika kuminya haki za watumishi wa umma!

NA RUSTON MSANGI. Mapema mwezi  Aprili na Mei 2017, serikali ilitangaza hadharani idadi ya watumishi wa umma wenye vyeti feki  (vyeti vya kughushi) na watumishi wanaotumia cheti kimoja kwa watumishi wawili na zaidi. Taarifa ya serikali ilisema watumishi takribani 9,000 wamegundulika kutumia vyeti vya kughushi, wakati watumishi takribani 1,000 wanatumia cheti kimoja watu wawili au zaidi. Sambamba na hilo la watumishi wenye mapungufu, Serikali ilitoa majina kwa kila mkoa ya watumishi waliohakikiwa na kuonekana wana vyeti halali kuanzia sekondari hadi vyuoni. Zoezi hili lilitumia muda na pesa nyingi za watumishi, pamoja na pesa za umma. Kipindi chote cha uhakiki, haki za watumishi wa umma hususani maslahi ya mshahara, madeni, nyongeza ya mwaka (salary increment), upandishaji wa madaraja nk. vyote vilisimama hadi sasa mwaka wa pili umetimia. Kwa mantiki hiyo hawa watumishi kwa ujumla nchini ambao wameonekana kuwa na vyeti halali baada ya uhakiki wa muda mrefu kufanyika na kukam