Posts

Showing posts from May, 2017

Ulipaji wa madeni ya watumishi wa umma, ufanyike kwa kasi kama uhakiki wa vyeti ulivyofanyika!

NA RUSTON MSANGI. Tangu serikali ya awamu ya tano iingie madarakani mwezi octoba 2015, takribani miaka 2 hadi sasa kumekuwa na misamiati maarufu kama UHAKIKI na UTUMBUAJI majipu. Hivi vyote vikienda sambamba kwa lengo la kuhakikisha watumishi wa umma waliopo makazini wana vigezo vyote ikiwemo kigezo kikuu cha kitaaluma. Lengo lake ni zuri japo ya mapungufu na usumbufu mkubwa uliojitoekeza kwa watumishi wa umma hasa wale waliokidhi vigezo vyote. Uhakiki umepelekea wengi kufukuzwa, kuacha kazi lakini na wengine kubaki kwenye nafasi zao. Uhakiki kwa watumishi wa umma ikiwemo walimu ambao ndio watumishi pekee wengi nchini kuliko kada yoyote ile, umesababisha usumbufu mkubwa sana hasa wa kiuchumi na haki nyingi za msingi za kisheria kusimamishwa, wakati watumishi wakiendelea kutimiza wajibu wao wa kazi katika majukumu ya kila siku. Mfano walimu wastaafu na waliostahili kupanda madaraja pekee wanaidai serikali zaidi ya bilioni 300. Mbali na usumbufu huu kwa watumishi wa umma n